Sunday, February 28, 2010

LOVE MESSEGES







2009 mwaka ndiyo huo umekwisha, mpenzi mola katuwezesha 2010 kutuonyesha nasi hatuna budi penzi letu kulidumisha, nakupenda na katu sitakutenda kwa mahaba matamu unayonilisha!

Hakika kuwa nawe nimefarijika, machozi yaliyokuwa yakinibubujika na machungu na makovu moyoni yaliyogubikwa yamefutia kwa mapenzi unayonipa, hakika nafarijika amini kwako nimefika kwa wengine katu sitapapalika!

Mpenzi najua umbali na upeo wa macho yangu, lakini nakuomba nitunzie mali zangu na katu usimpe mtu hizo zabibu zangu, amini daima u mawazoni mwangu, amini umeyapa thamani maisha yangu, nakupenda!

Kina napokumbuka miguno uliyonipa nabaki naweweseka, kiuno ulivyokata utamu maradufu uliongezeka, lavubiti uliyoniweka nikiitazama akili yanitoweka, nakupenda mpenzi utamu wangu kwa mwingine usije peleka!

Mara ya kwanza nilipokuona mwili ulinisisimka, nguvu ukaniisha maneno mdomoni yalitaka kunitoka lakini ghafla yalitoweka, tabasamu nikakuachia pale uliponikaribia, salamu uliponipatia nikazidi kuchanganyikiwa kwa sauti niliyoisikia, leo msg nakuandikia ukweli kukupasulia, nakupenda my dear!

Sielewi kwanini wanibania, ni muda mwingi nimengojea huruma kuonewa utamu kupewa lakini naishia maneno matamu kupewa na ahadi kupatiwa kuwa ipo siku nitapewa, nimechoka kungojea ukweli nataka kupewa kama penzi nitapewa au muda napotezewa!

Uliponifuata kwa mara ya kwanza na maneno matamu yaliojaa huba na uso wenye bashasha, shaka sikupata nikaamini mwanaume nimepata, ulichotaka sasa umepata chamoto nakipata, mawasiliano yamekata, asante sana wewe kaka.

Usiku mzima nimelala nikiweweseka kila maneno yako napoyakumbuka, siamini hivi leo umenigeuka, ahadi zote tulizoziweka leo wataka toweka, mapenzi moto niliyokupatia na kutwa hukuisha nisifia kwa ujuzi naokupatia leo wataka nikimbia, please dear usiniache mkiwa sema chochote nitakupatia!

Mchana umewadia wangu malkia hakikisha kitu kinywani chaingia, usiache hata kama kazi zimekuzidia kwani matatizo utakuwa wajitafutia, vidonda vya tumbo nafasi kuvipatia, nakupenda my dear please niliyokueleza zingatia!

Siamini macho yangu, nilikupa ruhusa ya kuufanya chochote mwili wangu, nikakupa hadi visivyohadithika, lakini mwanaume bado huonyeshi kutosheka, kila shimo wataka kuloweka, nakuombea heri na hao wenzangu mi’ niache na maisha yangu!

Hakika nimefarijika kwaraha jana ulizonipa, moyoni najiuliza ni mimi pekee raha hizi nayezipata? Tafadhali niondolee mashaka, akili yangu imewaka, wivu umenishika na mwili watetemeka! Nakupenda hny.

c)Brazatk 2010
Haki zote zimehifadhiwa hairuhusiwi kunakili kazi hii na kuitumia kwa shughuli za biashara kama kuchapisha kwenye magazeti, vijarida vya mapenzi au kutumia kwa namna yoyote ile yakujiingizia kipato bila kuwasilian na blog host!

No comments:

Post a Comment