Saturday, February 6, 2010

LOVE SMS kwa kiswahili

LOVE SMS
Sijui nikuekleza namna gani uelewe yaliyionijaa moyoni kwani kila nifikiriapo kwanini una walakini na hutaki kuniamini kama wewe pekee ndiye ninayekupa mahaba yangu makini, mpenzi rudisha yako imani ni wewe pekee nayekupenda hapa duniani!

Moyoni naumia kila napofikiria yale uliyonitendea, sijui nini nilikukosea kama mapenzi ya dhati naamini nilikupatia na moyoni nilikuwa najivunia na kujiona zaidi ya mfalme katika hii dunia kumbe kiini macho ulikuwa wanifanyia leo najutia muda ulionipotezea, kumbuka nilikupenda!


Nakiri kweli nimekukosea naomba msamaha kwa yote yaliyotokea hakika nimekukwaza lakini kwa kuwa hii ni yangu mara ya kwanza naamini utanisamehe la azizi na kunipa nafasi yakulienzi lako penzi.

Mpenzi nimekumiss jamani, sipati meseji wala simu sijui kwanini, nikikumbuka tunayofanyaga kitandani, natamani ungekuwa nami pembeni nakunipa mahaba yasiyo kifani, nakupenda si utani hani.

Nimezunguka pande zote za Tanzania macho nikiangaza kumsaka mrembo wakumkabidhi yangu nafsi na kulila tunda lake kwa nafasi huku nikimpa mahaba yangu ya dhati na sikuwahi kuhisi kama wewe ndiye ungeiteka yangu nafsi, nakupenda sweetie.

Ni yangu mazoe kila siku simu yako kuipokea kama si meseji kunitumia leo naumia kila napofikiria nini kimetokea hadi mawasiliano yetu yanaanza kupotea, enewei naamini hali ya kawaida itarejea na majonzi moyoni yatanipotea. Nakupenda la azizi.

Nina habari nzuri nataka kukwambia kuna mgeni leo kaja kunitembelea nguo nyekundu amevalia yaani utamu wako kwa sasa siwezi kukupatia maana mgeni huyu kashakuharibia, nakupenda dear.

U hali gani? Naamini mawazoni mwako upo nami japo yaweza kuwa hakuna ukweli wowote ndani, lakini nataka uamini kuwa umekuwa nami mawazoni japo sijawahi kukuona machoni.

Nakutakia kila la kheri katika maisha yako ya ndoa, wengi watakwambia maneno kila kukicha, lakini nakwambia wapo ambao kwa hakika watakaokuwa wamelenga kuitia doa yako ndoa, hangera rafiki yangu kipenzi kwani wengi wanaitamani ndoa lakini hawajapata wakuwaoa.

Mimi ni mzima japo si lazima kujua kama ni mzima lakini nachotaka kusema nashukuru Mungu kwakunijalia uzima na ni yangu matumaini u mzima na umejaa matumaini, mchana mwema.

No comments:

Post a Comment